Bei ya Betri za CWORKS Tanzania

Kama unatafuta bei ya betri za CWORKS Tanzania, huenda tayari unajua betri yako imechoka. Sasa unataka kujua betri mpya itakugharimu kiasi gani, na saizi gani inafaa gari lako.

Katika makala hii tumeweka bei za sasa za betri za CWORKS hapa AutoInc., kwa nini bei zinatofautiana kati ya saizi moja na nyingine, na jinsi ya kupata thamani ya hela yako.

Orodha ya Bei za Betri za CWORKS

Betri ya CWORKSBei (TSh)Magari Yanayotumia Kwa Kawaida
NS40L / NS40R135,000Magari madogo (hatchback na compact)
NS60L / NS60R170,000Saloon ndogo na za kati
N50L / N50R215,000Saloon za kati
N70L / N70R242,000Saloon kubwa na baadhi ya SUV ndogo
DIN66250,000Magari yanayotumia betri za saizi ya DIN
N100344,000SUV, pickup na magari ya dizeli
N90L354,000SUV, pickup na magari ya dizeli
N120L / N120R462,000Malori madogo, daladala na magari ya biashara
N200635,000Malori makubwa na mabasi

Bei kama zilivyo kwenye auto-inc.com, Septemba 2026. Bei na upatikanaji vinaweza kubadilika, kwa hiyo thibitisha kabla ya kufika.

Mifano ya magari ni mwongozo tu. Hakikisha kwa kuangalia kitabu cha gari lako au lebo ya betri uliyonayo, au waulize mafundi wetu.

Kwa Nini Bei Zinatofautiana Kati ya Saizi?

Sababu kubwa ni saizi na uwezo wa betri.

Betri kubwa inatumia malighafi nyingi zaidi na imetengenezwa kutoa nguvu zaidi ya kuwasha gari. NS40 ni kwa magari madogo, wakati N200 ni kwa injini kubwa za malori na mabasi. Tofauti hiyo ndiyo inayoonekana kwenye bei.

Je, Betri za L na R Zina Bei Tofauti?

Hapana. Hapa AutoInc., betri za CWORKS za L na R za saizi moja zina bei sawa.

Herufi hiyo inaonyesha tu terminal ya positive iko upande gani. Kuchagua upande sahihi ni muhimu kwa sababu nyaya za gari lako zimepangwa kwa upande fulani, lakini haibadilishi bei.

Je, Ununue Betri Kubwa Kuliko Unayohitaji?

Kwa kawaida hapana.

Watu wengi wanadhani betri kubwa ndiyo bora, lakini betri bora ni ile ambayo gari lako limetengenezwa kuitumia. Betri kubwa kupita kiasi inaweza isikae vizuri mahali pake.

Ila kama umeongeza vifaa kama taa za ziada, mziki au friji, au gari lako linafanya kazi nzito ya biashara, fundi anaweza kukushauri betri yenye uwezo zaidi ambayo bado inatoshea gari lako.

Unachopata Ukinunua Hapa AutoInc.

Bei ya betri ni sehemu moja tu. Ukinunua betri ya CWORKS hapa AutoInc., unapata pia:

  • Betri origino kutoka kituo cha magari kinachoaminika
  • Upimaji wa betri kuthibitisha kama betri yako ya zamani inahitaji kubadilishwa kweli
  • Ukaguzi wa mfumo wa kuchaji kuhakikisha alternator inafanya kazi vizuri
  • Ufungaji wa kitaalamu ili betri mpya ikae imara na iunganishwe ipasavyo
  • Ushauri kuhusu saizi na upande sahihi wa terminal kwa gari lako

Jinsi ya Kufanya Betri Yako Idumu

  • Weka terminal safi na zimekazwa vizuri
  • Hakikisha betri imefungwa imara
  • Zima taa na redio gari likiwa limezimwa
  • Mara moja moja endesha umbali mrefu kama mara nyingi unaenda safari fupi
  • Omba betri ipimwe kila unapofanya service

Joto la Dar es Salaam linapunguza maisha ya betri, kwa hiyo kuipimisha mara kwa mara ni muhimu zaidi.

Maswali Ambayo Watu Huuliza Sana

Betri ya CWORKS ya bei nafuu zaidi ni ipi?

NS40 ndiyo yenye bei nafuu zaidi kwa sasa, TSh 135,000.

Betri ya CWORKS N70 inauzwa kiasi gani?

N70L na N70R zote kwa sasa zinauzwa TSh 242,000.

Naweza kuangalia bei kabla ya kufika?

Ndiyo. Bei zipo kwenye auto-inc.com, au tupigie bure kupitia 0800 750 339 kuthibitisha bei na upatikanaji.

Bei inajumuisha ufungaji?

Uliza timu yetu ukifika. Tunaweza kupima betri yako ya zamani na kukufungia mpya kitaalamu.

Kwa kumalizia, bei ya betri za CWORKS Tanzania inaanzia TSh 135,000 kwa NS40 hadi TSh 635,000 kwa N200, kutegemea saizi inayohitajika na gari lako.

Hapa AutoInc., tutakusaidia kupata betri sahihi ya CWORKS, kupima betri yako ya zamani na kukufungia betri mpya kitaalamu.

Unataka kujua zaidi? Soma Sifa, Faida na Mwongozo Ukiwa Unanunua Betri za CWORKS, au tupigie bure kupitia 0800 750 339.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *